MUNZEZE WAHITAJI SOKO LA UHAKIKA LA ZAO LA MUHOGO

Maeneo mengi hapa nchini wanalima zao la muhogo kwa wingi kwa kuwa zao la muhogo ni zao ambalo linakubali mahali popote na lina uwozo mkubwa wa kuvumilia ukame kijiji cha munzeze kilichopo katika Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma  ni miongoni mwa vijijini hapa nchini vinavyo lima zao hili la muhogo kwa wingi.

Wakulima wa zao hili muhogo katika kijiji hiki cha munzeze wamekuwa wakitegemea sana zao hili kwa kuendesha mazao yao,changamoto kubwa wanayo kutana nayo baada ya kuvuna zao hili ni jinsi ya kuhifadhi kwani wamekuwa wakitumia njia duni katika kuhifadho mihogo yao. Continue reading

Advertisements

Wakulima wa kijiji cha Lusesa walilia maghala

Na Editha Karlo, Kigoma

Wakulima wa kijiji cha Lusesa Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma waiomba serekali iwajengee maghala ya kijiji  kwaajili ya kuhifadhia mazao yao ambayo yamekuwa yakiharibika na kuoza kila msimu unafika.hicho

Asilimia 99 ya wakazi wa kijiji hicho wanaendesha maisha yao kwa kutumia kilimo ambacho kilimo hicho bado kimekuwa hakina tija kwao.

Wakulima hao walisema kuwa wanapata hasara ya kuharibikiwa na mazao ya kwasababu ya kutumia njia za kienyeji za kuhifadhi mazao hayo.

Wakulima hao wameiomba serekali iwasaidie kuwajengea  maghala ya kisasa na vihenge ili wanapo vuna mazao yao waweze kuya hifadhi sehemu penye usalama.

Pia waliiomba serekali iwapatie dawa za kutunzia mazao ya wanapo ya hifadhi kwenye magunia ili wadudu wasiyabangue

fellow wa TMF akimsaidia mkulima wa zao la tangawizi kuchambua tangawizi iliyobora kijijini Lusesa

 

 

Hii blog ya habari za mikoani

Habari wapendwa hii ni blog ya mikoani tafadhali fuatilia habari za mikoani humu